Surprise Me

UCHAMBUZI: Korea Kaskazini, Kusini Wamaliza Bifu, Haijawahi Kutokea! - HDMaza.pw

Apr 27, 2018 3 0 1,037

UCHAMBUZI: Korea Kaskazini, Kusini Wamaliza Bifu, Haijawahi Kutokea! UCHAMBUZI: KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa ya Korea tangu vita vya Korea vya mwaka 1950-1953, ambapo ameingia Korea Kusini na kukutana na Rais wa nchi hiyo, ambaye amekuwa hasimu wake kwa muda mrefu, Moon Jae-in. Tukio hilo la kihistoria limetokea leo Aprili 27, 2018 ambapo tukio hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe na viongozi wa Korea Kusini na mwenzao wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa kushikana mikono katika mpaka huo kabla ya kukaribishwa na kuingia nchini humo. Hata hivyo shughuli zote za taifa la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili na baadaye watu walishangaa baada ya Kim kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshikana mikono. Viongozi hao walikagua gwaride ambalo likikuwa limevalia nguo za kitamaduni upande wa Korea Kusini ambapo wawili hao na baadaye walielekea katika jumba la amani huko Panmunjom, eneo la kijeshi katika mpaka huo ili kuanza mazungumzo yao. lnstal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Gl...... TWITTER: https://twitter.com/GlobalH... Visit https://globalpublishers.co..., Subscribe http://www.youtube.com/c/uw... kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uw... http://www.youtube.com/c/uw... http://www.youtube.com/c/uw... WEBSITE: https://globalpublishers.co... FACEBOOK: https://www.facebook.com/Gl...... TWITTER: https://twitter.com/GlobalH... INSTAGRAM:

eXTReMe Tracker
HDMaza.pw